WACHUNGAJI HAWAELEWANI KISA ATI “MAFUTA!”

Church Materials S/ No. 005

Fungu ya 5

WACHUNGAJI HAWAELEWANI KISA ATI ‘MAFUTA’

Leo nakuja kifingine. Leo nakaa ndani ya utumisi yangu. Leo nahubiri mahubiri yaliyojaa upako ya Roho Mutakatifu.

Kaeni kwa utukufu mkubwa kwa kuwa wale ambao hawajawahi kufunguliwa milango yao na madirisa silisofungwa na adui setani, sinaenda kufunguka.

Wale wako wamebeba milima sa matatiso balibali kama kukosa watoto, kukosa mitaji sa biasara, kuteseka na kesi sa kusingisiwa, mateso sa magonjwa na kila namna sa milima, leo Yesu menyewe anakwenda kusiporomosa hiso milima.

Hata sile makomeo sa mageresa, Yesu menyewe anakwenda kusifunja. Sio kwa sababu muko na stahili, la, ni kwa huruma yake tu. Sema amen kanisa!

Leo niko na hasira ya binguni. Nyuma pale naona mutu moja akiwa amefaa koti ya bluu na kiatu nyeupe, leather, uko na sida ya kodi ya nyumba, Bwana akupatie leo hii hii. Mtu mmoja aseme Amina.

Dani ya nyumba ya Mungu ndipo majibu ya sida setu yanapatikana. Tasama, dugu yule alikuja kwa kanisa, moyoni yuko na mambo mengi magumu lakini rohoni yuko na tumaini moja, yakuwa Yesu ni jibu la mambo yote. Pokea sawa sawa na imani ya roho yako na neno la Mtumisi wako.

Usiisi maisa ya masaka masaka. Masaka ya nini? Yesu yu hai. Amekaa kuume kwa Mungu Baba, akituombea.

Wakirisito, tembeeni kifua bele, mlimshuhudia kwa macho yenu akienda juu binguni kwa Baba yake. Fifyo hifyo ndifyo atakafyo rejea kuja kuwachukua. Kurie sida mkiku!

Katikati pale, naona mama moja uko na African native hair, uko umefaa kitenge ya West Africa, Bwana ananiambia uko na sida kama ya mama ya kwenye bibilia, aliyegusa kansu ya Yesu na kupokea uponyaji palepale. Pokea uponyaji yako sasa hifi katika Jina ya Yesu. Uko msima kabisa. Kanisa sema amina!

Leo Roho Mtakatifu anasema na Makanisa yote kupitia huduma hii.

Hebu tuangalie ile Warumi 8:5

Imeandikwa:

“Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.”

Masindano mingi dani ya huduma nyingi katika samba ya Bwana misingi yake ni WIFU ya kisetani. Na hii theolojia yake ni Watumisi saifu na ambao hawaisi rohoni bali mwilini – sawa na Warumi 8:5. Wao huufuata mwili na kuambatana nayo kana kwamba ni kitu ya kuchukuliana nayo wakati wote. Kumbe hiyo tendency imewanyima ngufu ya kiroho. Kwa kuwa waisio mwilini ni wa kimwili na waisio rohoni ni wa kiroho; tena husungumsa habari sa kiroho.

Sema amina kanisa!

Ngufu ya Mkiristo haiko mwilini bali rohoni. Ukitaka kuwa na ngufu ya kupambana na waganga na wachawi na kila adui katika ulimwengu wa mwili na roho, wewe isi rohoni. Wachawi mabingwa wa kutenda mambo ya uharibifu, wanatenda yote wakiwa rohoni zaidi kuliko mwilini. Kaa rohoni mutu ya Mungu, wakija mnakutana huko huko mnapambana kwa damu ya Yesu na tunguli. Acha kuisi kiasara asara mupendwa. Kuwa askari hodari ya Yesu ukiamini katika ngufu na uweso wa Yesu Kiristo.

Kanisa sema amina!

Mkiristo anayepinga mafuta hasa mutumisi, anatia masaka katika utumisi yake. Anaonekana ni mutu yuko yuko na kiroho kinyonge kinyonge kilichogubikwa na misimu ya kwao huko Giriama au kule kwetu Turkana!

Kwanini unapinga mafuta wewe? Pengine ungenitia moyo kama ungepinga fesa kufamia ndani ya kanisa. Kwamba sasa, huduma dani ya kanisa simegeuswa bisaa. Karubu sitawekwa na Amason kama sio Kelsoko.

Bisaa hisi, nasungumusia sile anbaso musingi wake ni Yesu Kiristo tu. Siko huduma ambaso musingi wake ni Setani. Hisi sa Setani, hasinihusu kwa kuwa mimi sijui mambo sa Setani. Najua habari sa Yesu Kiristo tu.

Neno ya Mungu inasema, umepewa bure… Toa… Bure. Hawa Yesu anawaangalia na anatunsa hesabu sao, watakutana ofisini. Ninyi kondoo sa Yesu, kuweni wapole, toeni mapato yenu ya haki kwenye mikono mipotofu, nayo hatimae hugeuka kuwa sambi ya mauti. Kweli yote imo dani yao hao waalimu wa imani, lakini wamekaidi maagiso ya bosi wao – Yesu! Wameipenda dunia na fesa kuliko Neno ya Mungu wao. Ole wao…

Mutumisi anayekosa mafunuo ya kwake menyewe…huansa kusambulia mafunuo ya watumisi wengine. Huyu anafanana na Yuda Isiarioti… Yuko na broken heart!

Yuda Iskarioti, Bwana amrehemu, inaonekana alipenda sana fesa. Inawesekana mahali fulani alitaka kumpindua Yesu ili achukue nafasi yake atengenese fesa saidi. Mupendwa, unajua fesa inatengeneswa? Sema amina!

Basi, Yuda alipoona hawesi kumupindua Yesu kutokana na ile ngufu alikuwa nayo na kiasi ya malaika inayomsunguka saa 24, akaangalia samani yake, akaona ni kubwa, akaamua amuuse. Yuda alikuwa mutu ya mwilini asilimia mia. Hifyo, alimuusa Yesu musima musima kwa fipande 30 fya fesa. Nakemea roho hii ya utapeli isiwe dani yenu katika Jina ya Yesu! Kanisa sema, amina!

Yuda angekuwa mutu ya kiroho, angemuusa Yesu kiroho (God forbid). Leo, hapa iko watu imekaa nasi lakini samani yote haimo dani yenu, imeibiwa. Nyota siro, hamuna. Kibali, siro, hamuna. Ndoto, siro, hamuna. Ubunifu, siro, hamuna. Kila kitu wameiba, wameusa huko kwa wafayabiasara, wanasiasa na mastaa wa musiki..

Leo kama Bwana aisifyo milele, nasema, pokea kila kilicho chako toka kwenye mikono ya adui kwa Jina ya Yesu Kristo. Na ninafunika neema na baraka sako kwa Damu ya Yesu Kristo. Kanisa sema, amina!

Tuangalie ile Mwanso 28:18 – 22

Mwanzo 28:18

“Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.

Mwanzo 28:19

“Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.

Mwanzo 28:20

“Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;

Mwanzo 28: 21

“nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.

Mwanzo 28: 22

“Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”

Kumbe muasisi wa fungu ya kumi ni Yakobo! Tunaamini hifyo kwa kuwa haya yanaripotiwa katika kumbukumbu sa kitabu cha Mwanso na Mussa. Je, unajua ya kuwa fitabu fitano fya Mwanso fyote mwandisi wake ni Mussa? Chukua hiyo sasa.

Yakobo anatumia mafuta kutakatifusa jiwe; akiliondoa katika asili ya uharibifu na kulihuisa; kulifanya kuwa chombo kitakatifu kwa ajili ya BWANA na kwa ajili yake na fisasi fyote.

Kupitia ngufu ya mafuta haya, mji mpya Betheli unasaliwa, mahali ambapo inajengwa nyumba ya BWANA kwa ajili ya kumwabudu Mungu wa binguni katika Roho na kweli.

Mafuta ya upako, mafuta yenye ngufu sa kibingu yanaruhusu maono mapya ya kutengenesa usirika mtakatifu na Mungu kupitia kasi sa mikono yetu.

Ahadi mpya baina ya Yakobo na Mungu inawekwa, nayo ndiyo hii: kumtolea Mungu moja ya kumi ya mapato yetu yote kila yapitapo mikononi mwetu; kama msingi wa kulinda na kutakatifusa tisa ya kumi iliyosalia ili nsige, tunutu na madumadu wasile.
Kanisa sema, amina!

Tuangalie Kutoka 40:9

Ambapo Mungu anamwagisa Mussa kutwaa mafuta matakatifu; mafuta ya upako na anamwambia ya kwamba:

“Kisha utayatwaa mafuta ya kutiwa, na kuitia mafuta hiyo maskani, na kila kitu kilicho ndani yake, na kuiweka iwe takatifu, na vyombo vyake vyote; nayo itakuwa takatifu.”

The work of proper annointing oil is nothing but annointing by sanctification. However, if not well prepared and used based on inner faith, nothing manifests. Unless is something else more than annointing oil which the genesis of it is the Holy Spirit. Not everyone can prepare annointing oil, no! Annointing oil is a SACRED sacrament ANNOINTED by the Holy Spirit. It is called annointing oil because it has been ANNOINTED by the HOLY SPIRIT. Something very valuable.

Upo hapo mupendwa, au kisungu kinasungusa kichwa yako? Pole, nakutia hasira takatifu uende sule ya kisungu. Mbona mimi nasoma kiswahili huko BAKITA?

Pale juu Mungu amempa Mtumisi yake Mussa maelekeso jinsi anawesa takasa hema ambamo ndani yake imo Masabahu na fitu fya kutumika katika patakatifu. Mussa anatii na anafanya hifyo.

So, Mutumisi ya Mungu anapatia kondoo sake fyombo fitakatufu ili fitumike kupambana na ngufu sa gisa popote watakapokuwa. Anawapa kwa Jina ya Yesu baada ya kuwafundisa, hawapi kama hirisi. Anawapa wakiamini. Wale wanaoamini tu, ndio wanaonufaika na fitakitifu hifi. Sida iko wapi wapendwa?

Kila kitu ambayo Mungu ameumba kwa Neno yake menyewe, ni takatifu na dani yake imo ngufu. Tumeona JIWE ya Luzu iliyobadiliswa jina na kuitwa Betheli, palipojengwa nyumba ya Mungu.

Punda ya Balamu iliongea, fimbo ya Mussa ilimesa fimbo sa wachawi, fimbo ya Mussa iliigawa bahari, mate ya Yesu na udongo ilifungua macho ya kipofu, maji ya mto ilimponya jemadari ya jesi ukoma, chupa moja ya mafuta mama ya Serepta ilijasa mapipa, maji iligeuka difai katika harusi ya Kana, samaki alimupatia Petero fesa ya kulipa kodi yake na Yesu, lakini hata maji ilifanyika barabara Yesu na Petero wakapita juu yake. Maana yake nini? Kila kitu ni mutumisi ya Mungu.

Mutu ya Mungu sema, kila kitu ni Mutumisi ya Mungu hata setani ni Mutumisi ya Mungu.

Kwa hiyo, kuyahukumu mafuta, chumfi au vitu balibali, huo ni usamba tena usamba ya Setani!

Unahitaji utafiti tena ya kina ku-attack subject ya mafuta na fitu singine sa namna hiyo. Mimi sitetei wahuni wahuni wanaofikiri church ni mahali pa kutafuta maisa, no! Hapo ni usaifu wa mamlaka kasaa. Sitaki niingie humo.

Najua mpaka hapa hakuna sida. Sida iko hapa, kwanini watose fesa, faranga, mbongo, makuta, money? Iyo tu!

Sasa wewe ulitakaje? Wapewe bure? Ungekuwa ni wewe baba mtumisi, ungetoa bure? Na hii mafuta sio mafuta ya korie au aliseti. Ni mafuta ya mseituni toka Israel… Ungetoa bure? Chumfi sio ya Bahari ya Hindi ya majini, ni ya Israel. Hata ingekuwa ni tangawisi ya Same, bado ungenunua na ungesafirisa. Bado utoe bure? Au mnafikiri Bill Gate ako ana-finance hisi suhuli sa makanisa? Huku Bill Gate hana mukono!

Mbona hamlalamiki cd, DVD sa kwaya na mahubiri, fitabu vya watumisi hafitolewi bure? Katika fyoote mmeona mafuta, chumvi, fitambaa, kalamu, kalenda, writsband, asali nk? Sitakuja siku sijaso na sukari, sabibu, ndisi, pipi, mayai, mikate, nsige hata masiwa na pilipili. Kwani sida ni nini?

Yohana Mbatisaji, aliisi porini akifunga na kuomba akila nsige na asali mwitu, basi. Mafunuo yake tayari yameingia kanisani, bado nsige na senene!

Yakobo ali-annoint jiwe, unakumbuka hiyo Mwanso 28:18. Mbona hamlalamiki kwanini alitumia kitakatifu juu ya jiwe kitu cha hali yachini? Nakwambia, tena nawatuma waambieni wa nyumbani mwenu waje wamebeba jiwe, litieni mafuta matakatifu wakasimike pale wanapotaka kujenga makasi sao. Majengo yao na miji yao ipate kusimama imara. Wala hakuna adui atakayewesa kuigusa milele. Hata ile miji iliyokwisa kusimamiswa, wainue jiwe lililotiwa mafuta na kusimika katika miji yao ili iungane na Betheli hata milele.

Maono yanapatikana toka katika Neno ya Mungu pamoja na usirika wako na Roho Mtakatifu kupitia mafunuo…

Watumisi muko na mambo mingi. Muko na miradi. Muko na masimu na mafesi buuku. Muko munakata mitaa huku na huko. Muko munahangaika kufuatilia huduma ya huyu na yule. Huduma ya yule inakuhusu nini wewe? Hata kama anamhubiri setani laifu, inakuhusu nini wewe? Umeitwa kupambana na wachungaji wengine au kusugulika na kondoo sako ulisotengewa na Bwana?

Please, be serious. You are too gossipers some of the so called men of the Most High. Why? For what? Focus on your ministries.

Kitu ambayo natambua kabisa ni genuine kwa wachungaji, ni namna ya kuendesa huduma. Kwa kweli ni changamoto inayopasua kichwa ya wachungaji wengi hasa wachanga.

Wako watumisi wengi ambao Mungu amewaita katika ukamilifu wote. Bado hawajaingia ndani ya game kwa sababu namna ya kuansa huduma ni changamoto kwao. Mistake yao ni hii: wanataka waansie huduma dani ya nyumba. A nice place, with music set, lights etc. Rafiki, utachelewa sana kama Yona. Yona alikuwa anasubiri ndege impeleke Ninawi. Alipoona haipatikani, akaamua aende sake Tarsisi akafanye biasara ya kuusa sanaki kwa meli.

We, acha kabisa. Mungu akiita, ameita. Mungu akikupa, amekupa. Haikuwa sida kwa Mungu. Unajua ile sanaki ilimesa Yona, ilikuwa pale miaka mingi. Ile sanaki ilikuwa na usoefu wa kumesa wafufi wakorofi walioingilia anga sake kwenda kupungusa samaki sake ambaso ndiso silikuwa chakula yake katika msunguko ule.

Ile anasuswa tu baharini, wala hakufikia maji, no, alidakwa juu kwa juu wala watupaji hawakujua kama pale big fish alikuwa around. Wangemwona, hakika nakwambia wangehairisa mupango yao ya kum-throw Yona kwa maji, maana, fish alikuwa so big!

Mungu mwacheni aitwe Mungu tu. Ile anaingia tip kwa tumbo ya ile sanaki ikiitwa nyangumi, mara tap, Mungu akafunga sile pipes sa kuachilia ile sumu ya kuyeyusa chakula. Unajua nikwambie, ile samaki ili – suffer kitu kitaalamu inaitwa ‘Acute constipation.’ Yaani, the food is not digested at all!

Samaki ikarukaruka, no digestion. Ikaenda hadi Ninawi (I think it was a prophetic fish), Ikaenda hadi Tarsisi na miji mingi, fast and slow, no digestion!

Yona akagundua kitu, he is not digested in time. Akatambua Mungu hajamwacha. Akafanya toba ndani ya tumbo ya samaki. Akalia sana. Akamwomba Mungu amsamehe. Akaahidi akipata second chance, ataenda Ninawi akafanye kasi ya Mungu. Mungu akamsikia Yona toka ndani ya tumbo ya samaki. Akamsamehe! Akamwamuru samaki akamtapike Yona Ninawi. Na ndifyo ilifyokuwa!

Wewe mupendwa, hiyo tabia mbofu ya kutongisa wake sa wensio, huachi mpaka umeswe na nyangumi?

Watu wa Ninawi walikuwa wa ajabu sana. Sema amina kanisa. Wale Waninawi walikuwa wanaabudu Mungu Samaki. Mchana kweupe, tena siku hiyo kama ilipangwa file. Walikuwa wamejaa huko ufukweni. Yule samaki kutokana na msukosuko wa ile accute constipation, aliibukia pwani ile na kumtapika Nabii Yona ‘pwaaa’ hadi kule nchi kafu! Hifyo hifyo na malenda malenda ya tumbo ya samaki, Yona akaansa pale pale kasi ya kufikisa ujumbe ya Mungu kwa Waninawi:

“Watu wote wa mji wa Ninawi, mnisikie.. Mimi Nabii Yona, Mungu ako anasema, tubuni, acheni sambi. Msipotubu, upesi atauangamisa mji kwa moto kama Sodoma na Gomora. Tubuni… Tubuni… Ninawi… Tubuni!”

Kwa sababu alitoka kwenye kinywa ya samaki, na sehemu kubwa ya watu imesuhudia kwa macho yao wenyewe…

Upesi watu wakaambiana… Habari ikawa kubwa, ikafika hadi kwa Mfalme kupitia kwa maafisa usalama… Mfalme alipothibitisa neno lile, akaagisa watu wote katika nchi, wakubwa kwa wadogo hadi wanyama, wafunge siku 3 bila kula, wakiomba na kufanya toba. Hata Mfalme alijipaka majifu, akafunga, akamlilia Mungu, Mungu akamsikia toka patakatifu pake, akawasamehe!

Nsuri-i-i?

Watu wa Afrika Mashariki tunajifunsa kitu gani hapa? Tumeona Mfalme wa Tansania alifyopambana ka CORONA, kama Mfalme wa Ninawi. Na Mungu aliacha hayo mataifa jirani yateseke makusudi. Wafalme hawa wamesindwa nini kuiga kwa Mfalme mwensao na kuamuru watu wao kumgeukia Mungu kama jibu pekee kwa tatiso la CORONA? Oh, hatuwesi iga! Ok, hamuwesi iga, at least, copy! Na hiyo nayo mnasindwa? Au style ya TZ ya maombi ya CORONA ilikuwa na copyright? Na kama ina copyright, sida iko wapi, kuomba kibali? Leaders, you are not serious with the welfare of your people!

Neno ya Mungu inasema, mambo ingine haiwesekani pasipo kufunga na kuomba. Watu wafunge na waombe. Taasisi sifunge na waombe. Nchi sifunge na siombe. Sida iko wapi? Kule Singida wanasema, ” Kurie sida Mnyampaa!” Yaani, hakuna sida baba!

Kwa hiyo narudia tena. Ninyi Watumisi wachanga msiige kila kitu kwa wakongwe. Huwesi amini, wakongwe wengi wako nje ya geti ya Mungu. Mungu amewatenga wala hana habari nao. Wako tu wanajiendea kama kipofu. Katika madhabahu sao, Mungu hayupo. Wanaabudiwa na kutukuswa wao!

Children of God, the days of reckoning are coming. We shall know who are truly SERVANTS of God and who are not!

Maisha yao ni mfano rahisi. Maisha ya kifahari. Wapenda fesa, sifa na utukufu. Usiwaguse. Hawataki hata Serikali iwaguse, hata kama wanakosea. Wanakiburi na jeuri. Hii si tabia ya Mtumisi ya Mungu. Mtumisi ya Mungu ni mnyenyekefu. Ni mfumilifu. Anachukuliana na hali sote. Kubwa kuliko yote, ana UPENDO.

Inawesekanaje, unawachangisa waumini yako miaka kumi, unadai kujenga jengo ya ibada na jengo ya ibada haionekani. Pesa sote sinawekwa kwa akaunti binafsi ya jina yako mwenyewe, ikisidi sana na mkeo. Ila wewe, unabadilisa magari ya kifahari. Unafaa suti sa bei kubwa. Unajenga nyumba sako binafsi hadi sa kupangisa. Hoteli sote kubwa kubwa unajulikana. Hii maneno iko sawa kweli?

Hapa iko Roho wa Mungu na upendo ya Mungu? There must be a serious problem if not a mistake!

Bwana YESU asifiwe! Nimeisa toka nje ya mada. Anyway, yote ni kwa utukufu ya Bwana Yesu!

Let me stop here, I feel disorganised!

Pamoja na maneno mingi hapo juu, wacha nitengenese samari ya kichwa ya habari.

Mafuta isifuruge kanisa. As long Bible is the universal point of gathering the Word of God and the Bible is standard.

I don’t doubt the Genesis of annointing oil discussed here. If by the way, the Genesis of the annointing oil supplied in the churches are different from different sources that it’s origin doctrine is not the Bible, then, there is a serious danger as far as annointing oil is concerned.

By the way, charging to the members of the church should not behave like a business kiosk. That is extremely far far away from the guidelines given by the Bible. Free you have been given, free you shall give. That is according to the scripture.

Most churches are now in the business row without paying tax. Another sin the church is committing.

This should be taken seriously. Mamlaka sinaso simamia mifumo ya Ukristo katika nchi anbaso hii ‘business’ is serious, they must act accordingly before we are supplied with annointed ‘locusts’ of John the Baptist!

And if that is not enough, they will begin to bring the stones from Israel referring Jacob’s scripture in Genesis 28:18 – 22.

Glory to God, church!

Pst. Anyango Anyango, PhD

Tuonane Fungu ya 6, fungu ya sita itakuwa ni ‘fire!’ Nitatupa mawe kweli kweli. Nataka nimponde setani na semeji sake sote… And that is my job I’ve been born for!

© Presenter:


Abraham Blessings, DSM