UNATAKA KUMUPENDESA KILA MUTU

UNATAKA KUMUPENDESA
KILA MUTU

Church Material S/No. 004

Fungu ya 4

Kama unafikiri wewe uko na roho nsuri sana, kwanini usikatise mbuga ya Mikumi kwa muguu tena usiku ili Mr. Lion na mkewe Mrs. Lioness wawese kujipatia ‘supper!’ Halafu wewe kwa sababu you have good heart and love, uende binguni ukaketi na Ibrahim na Lasalo. Why not? Because is stupidity!

Kama huwesi fanya hiyo maneno hapo juu kwa kuwa ni upuusi, why, unakuwa mutu rahisi rahisi kwa watu, ati jamaa, huh!

Utakimbiwa na muke wewe muchana kweupe! Focus on your family: just papa and mummy, wife and children stop! Wadogo sako au big brothers and sisters, they are not your kids. They have their own papa and mama. If your papa or mama asks you, that is a different ‘menu’ all together.

Subiri mutu ya Mungu, leo sihubiri. Niko na hasira bila saka ni ya Roho Mutakatifu.

Tasama, familia yako hakuli fisuri. Familia yako mwenyewe, sio ya kukodi, hapana. Familia yako mwenyewe, hafai fisuri, kisa ‘extended family!’ Are you in your mind or in Kiambui’s witch doctor calabash?

Inatakiwa uende kwa Dr. Ben Carson akague nerves sako, inawesa kuwa iko tatiso pahali. Sio bure!

Leo nitajitahidi kuminya kisungu au ung’eng’e. Ila hasira ya Roho Mutakatifu ikipanda tu, najikuta tayari niko nimemwaga kisungu. Niombeeni huyu pepo ya kisungu isindwe na itokomee huko huko Machakos…au pengine ni ya Murang’a, mimi sijui…

Kitu ingine, hii kiswahili yangu ina ‘Plaster of Paris – P.O.P,’ usije ukaiga. Iko na sida. Nimesema niko kwa ndarasa ya kiswahili BAKITA, therefore, usinipeleke kwa fyombo fya seria, ati oh, PhD holder anatianaga mambo hasieleweki na kiswahili. Hii kiswahili ni ya hapa hapa, iache hapa hapa. Sungumusa kiswahili yako musuri. Nami niko kwa njia… Usichese na kiswahili, utafungwa. Sitaki kwenda mageresa kula Sima ya kupimianaga! Mimi sima nakamata, kama hatosi naambia Mama Ntilie, sorry, Mama Lise, ongesa! So, take care!

Naachana na hiyo maneno. Naenda kwa maneno ingine ya kifamilia kama ile ingine. Hii iko complex, namaanisa ngumu kidogo kusimulia. Ila, ni ya kweli milele!

Familia moja huko Kakamega, ilikuwa na watoto 14. Just imagine fourteen, mama moja, baba moja! Anyway, sio tabu sana baba moja, lakini hebu fikiria, mama moja, fourteen! May Jesus bless this mama!

Mungu namupenda sana. Kama ilifyoandikwa kwa bibilia, kwake, siku moja sawa na siku alufu moja. Lakini tena, astonishingly, siku alufu moja, sawa na siku moja. Ai!

Tena maajabu ingine, yeye huwesa kuansia jambo bele akarudi nayo nyuma. Au akaansia nyuma akamalisia nayo bele. Mungu ni Mungu tu, jina yake itukuswe milele! Sema amina!

Kaka mukubwa alifanikiwa kusoma chap chap. Akabarikiwa kupata kasi chap chap. Sema chap chap mutu ya Mungu ubarikiwe. Nami nakuombea kipawa ya kufanikisa mambo sako sa baraka chap chap. Sema amina ubarikiwe!

Hii kaka mukubwa, I mean, first born, ilikuwa na upendo mingi. Upendo ile kisungu inaitwa, upendo ya AGAPE, I believe so, sifikirii alikuwa akiugua ugonjwa ya akili au baba alimuloga, sifikirii.

Na hapa ndio nataka ansia stori yenyewe. Hii stori ni big story. Iko na kitu nataka mutu ajifunse. WARNING: I don’t teach people not to LOVE their family members especially brothers and sisters. No! Take note. Nakufundisa uwe na akili. Nakufundisa kuansa na familia yako kwansa. God did not brought you here on earth to be a good samaritan. But a father or a mother.

Mutu ya Mungu sema amen ubarikiwe!

Sasa sijui ni setani au ni malaika ya Bwana ilimusauri au ni misimu ya kwao, mimi sijui. Najua kitu moja tu, alisimamisa kila kitu akaweka big promise ya kuansa kusomesa wadogo sake moja baada ya ingine hadi University. Wow, what a big job! Na kwa sababu hiyo, alisitisa mupango ya kuoa mapema. Sababu, amusaidie babaake kusomesa watoto yake 9. Hii 4 including yeye baba alikwisa somesa.

To make a story short, by the time anamalisa mudogo yake ya mwiso, I mean, anamalisa kusomesa university, sio A-Level, he was already an elder, musee, ameseeka, imagine! Ndio anakumbuka kujenga na kuoa. By the time anapata mutoto ya kwansa, ya pili na ya tatu, retirement hii hapa kwa mudomo, yaani kustaafu inagonga hodi chap chap!

Mutu ya Mungu, fungua masikio na mudomo nikusimulie… Sema, simulia mutu ya Mungu!

Angalau nyumba aljenga ya hifyo hifyo. Si baya. Kimbembe kusomesa watoto. Akikorogea brother hii simu imu- support school fees, inatia-excuse nayo iko inapambana na mambo ya ada ya watoto yake. Anaacha hii anapigia sister ile, nayo inatoa excuse, husband amekataa hiyo maneno.

Hii musee…at the end ilipata stroke…ikakufa, ikaacha watoto wadogo yatima without education, without future… Just imagine!

Natoa hii stori, not to kick the door of becoming a good samaritan. Even Jesus was a good samaritan. He fed over 5000 men and a number of women and children without asking them a coin. He was a good samaritan. Become a good samaritan. Assist people around you but with brain and consciousness alerted!

Aisee, kimombo ina-flow kama Michael Schumacher kwenye Formulae One. Hatari!

Baya kuliko yote, no brother or sister adopted any of the children to support them the way they were supported… Mbaya-e?

Kule Dodoma kibiriti ikiisha, wanasema, ‘Chibiriti chamarika!’ Na wewe usisubiri Hadi ‘kasi yamarika!’ Ndio uanse kuwa ngumu wa pesa sako. Pesa ni roho. Pesa iko na masikio. Tumia kwa faida ya familia yako.

Acha ubwege wewe, angalia familia yako kwansa. Charity begins at home!

Mutu ya Mungu, mwenye masikio na asikie!

Don’t miss Part 2

Pst. Anyango Anyango, PhD

Tuonane Fungu ya 5

© Presenter:
Abraham Blessings